Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba adaiwa kumbaka mwanae wa kumzaa

RPCDebora 660x400 Baba adaiwa kumbaka mwanae wa kumzaa

Wed, 30 Sep 2020 Chanzo: millardayo.com

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia mkazi wa Mtaa wa Kambarage Manispaa ya Shinyanga Petro Maro (43) kwa tuhuma ya kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 13 Mwanafunzi wa Darasa la Saba.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema kuwa Petro alitekeleza tukio hilo Septemba 27 majira ya usiku nyumbani kwake.

Amesema kuwa Mama Msamaria mwema anayeishi jirani na Petro aligundua  binti huyo kubakwa na baba yake Mzazi na kisha kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ambao walifika na kisha kumkamata.

“Binti huyu alibakwa na baba yake usiku akiwa amelala na chanzo cha tukio hilo ni tamaa za kingono baada ya kutengana na Mke wake hali iyosababisha kuendelea kuishi na mwanae wa kike nyumba mmoja” Magiligimba

Kamanda Magiligimba ametoa wito wananchi mkoani humo kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili kukomesha matukio na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto mkoani humo.

Ameongeza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtuhumiwa huyo na upelelezi ukikamilika atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.

DUUH! NDOA IMEVUNJIKIA HONEYMOON, BIBI HARUSI ALIALIKA MCHEPUKO WAKE HARUSINI

Chanzo: millardayo.com