Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba adai kumpa pesa mwanaye kujenga ghorofa linalogombewa

Gorofa Pic Data Ghorofa linagombewa kati ya Tuwaha Muze (44) na aliyekuwa mkewe Maimuna Soka.

Tue, 17 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Samson Tuwaha (71) ambaye ni shahidi wa pili wa upande wa utetezi katika kesi ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo mahakamani, ameieleza Mahakama kuwa Julai 2013, alimnunulia mwanaye (Tuwaha Muze) kiwanja na hatiame kujenga nyumba ya ghorofa moja eneo la Mbezi Luis.

Samson aliyewahi kuwa mfanyakazi wa wizara ya Viwanda na Biashara na mwanae Tuwaha Muze (44), wanakabiliwa mashtaka mawili katika kesi ya jinai namba 186/2019, iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Katika mashtaka hayo, Muze na baba yake wanadaiwa kughushi makubaliano ya uongo ya upangaji wa nyumba, wakionyesha nyumba hiyo ya ghorofa moja iliyopo Mbezi Luis ni mali ya baba yake mzazi na Muze, Samson Tuwaha, wakati wakijua kuwa ni uongo.

Shtaka la pili, Muze na baba yake mzazi wanadaiwa kuwasilisha mahakamani nyaraka za uongo za mwenendo wa kesi ya takala (ndoa) namba 66 ya mwaka 2017, katika mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, wakati wakijua nyaraka hizo ni za uongo.

Katika maelezo yake ya ushahidi alioutoa jana Mei 17, Samson amedai kuwa kiwanja hicho kilikuwa na thamani ya Sh11.5 milioni na kwamba alitoa fedha zake kutoka katika akaunti yake katika benki ya CRDB, tawi la Lumumba.

Related Wanandoa wagombea ghorofa, mume adai ni la baba yakeAdvertisement Akiongozwa kutoa ushahidi wake na wakili wa utetezi Alexander Mzikila, shahidi huyo amedia mwaka 2012, alimwitwa mwanae nyumbani kwake na kumkabidhi eneo kwa ajili ya kuchimba kisima cha maji.

Samson alikuwa akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Romuli Mbuya, wakati shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya washtakiwa kuanza kujitetea baada ya kukutwa na kesi ya kujibu.

"Nilimruhusu kijana wangu kuchimba kisima cha maji katika nyumba yangu iliyopo Mbezi Luis kwa njia ya maandishi, Desemba 16, 2012 na Julai 2013 nilimnunulia Muze kiwanja kwa mkopo wa Sh11.5 milion.

“Fedha za ununuzi wa kiwanja hicho nilizpata wakati nafanya kazi Wizara ya viwanda na biashara mkoani Tanga ambapo baada ya kununua viwanja hivyo nilijenga nyumba ya ghorofa eneo la mbezi Luis Dar es Salaam," amedai Samson.

Amedai nyumba hiyo alimkabidhi mtoto wake wa kiume aitwaye Tuwaha Muze kwa makubaliano ya kuishi kwa muda na aliyekuwa mkewe.

Shahidi huyo ameomba mahakama hiyo ipokee risiti za malipo ya benki alivyofanya wakati wa ununuzi wa kiwanja hicho, jambo ambalo upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa Serikali Adolf Verandumi ulipinga kupolewa kwa nayaraka hizo kwa madai kuwa shahidi sio mfanyakazi wa benki na nyaraka hizo hazina uthibitisho wowote kama zimetoka benki ya CRDB.

Baada ya upande wa mashtaka kupinga nyaraka hizo, shahidi huyo ameomba kuziondoka katika ushahidi na hivyo kuendelea kutoa ushahidi wake.

Pia shahidi huyo alikiri kuwa licha ya nyaraka hiyo kuwa na saini yake lakini hakuwepo wakati nyaraka ya makabidhiano ya nyumba inafanyika.

Alipoulizwa na wakili wa Serikali kama anafahanu hukumu ya ndoa iliyotolewa Mahakama Kuu ambayo iliruhusu mwanae na aliyekuwa mke wake wagawane mali walizochuma wakati wakiwa katika ndoa, shahidi huyo amedai kuwa taarifa hiyo ameisikia jana mahakamani hapo.

Pia amekiri kuwa alitoa fedha kwa mwanae ili amnunulie kiwanja lakini mwanae baada ya kununua kiwanja aliandika jina lake Tuwaha Muze na sio jina la baba yake (Samson Muze).

Alidai kuwa siku anakabidhi mali za familia, nyumba hiyo aliyodai kuwa ni ya kwake ilikuwa na jina la Tuwaha Muze na sio Samson Tuwaha.

Akiendelea kumhoji shahidi huyo kuhusiana na ushahidi aliyoutoa, alimuuliza kama anakumbuka Muze katika ushahidi wake alidai kuwa akikabidhi nyumba hiyo kwa familia na sio kwake?

Akijibu swali hilo, Samson alidai kuwa yeye ndio familia.

Samson baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake, Hakimu Mbuya aliahirisha hadi Mei 18, 2022 itakapoendelea na upande wa utetezi kuja na shahidi mwingine na washtakiwa wapo nje kwa dhamana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live