Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Amuua Mwanaye na Kumtupa Kwenye Korongo

RPC NJOMBE HAMIS ISSA.jpeg Baba Amuua Mwanaye na Kumtupa Kwenye Korongo

Sat, 5 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JESHI la Polisi Mkoa wa Njombe linamshikilia Ambwene Sanga (34), ambaye ni baba wa kambo wa mtoto Mesia Kaduma (5) pamoja na mwenzake Marko Mbilinyi (32) wakazi wa Imalilo, wilayani Wanging’ombe kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mtoto Mesia na kumtupa korongoni.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema; “Huyu Mtoto wa Kambo anasoma Shule ya Chekechea Imalilo, alipotea na alivyopotea akawa anatafutwa mpaka Serikali ya Kijiji ikahusisha wanafunzi na wanakijiji kumtafuta.

"Ndipo mtoto huyo alipokutwa korongoni akiwa amekatwa na ana majeraha makubwa tisa kwenye kichwa chake na wadudu kama sisimizi na siafu walishapanda mwili wake na kujipatia chakula.

"Jambo la kushangaza na baba wa kambo wa mtoto huyo aliungana na wananchi kwenye msako wa kuutafuta mwili wa mtoto huyo wakati ni miongoni mwa waliohusika na maujai, hii ni roho mbaya ama ni chuki huwezi kusema ni wivu wa mapenzi kwasababu mwanamke aliyekuwa naye tayari alikuwa amemzalia mtoto.

Kamanda Issah amesema Jeshi hilo linatarajia kuwapeleka Mahakamani watuhumiwa hao pindi upelelezi uatakapokamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live