Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ayubu atupwa jela kwa kulawiti mtoto wa miaka 6

Ayubu Kiyanza Ayubu atupwa jela kwa kulawiti mtoto wa miaka 6

Tue, 27 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha maisha jela Ayubu Kiyanza (22) Mkazi wa Don Bosco Manispaa ya Iringa kwa kosa la kumlawiti Mtoto mwenye umri wa miaka 6 aliyekuwa akisoma darasa la pili.

Mtuhumiwa alitenda kosa hilo November 01, 2021 na alimvizia Mtoto huyo akiwa anatoka Shuleni ndipo akamvuta kichakani huku akiwa amemziba mdomo ili asipige kelele.

Baada ya Kufika nyumbani Baba yake alimuona Mwanae akiwa mchafu tofauti na alivyomzoea akitoka Shuleni na ndipo akamuhoji na Mtoto akamueleza Baba yake kilichotokea na alimwambia Mwanae ampeleke eneo alilofanyiwa ukatili, wakiwa njiani walimuona Mtuhumiwa Ayubu Kiyanza na taratibu za kumkamata zikafanyika.

Akisoma Hukumu Hiyo Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa Rehema Mayagilo amesema Mtuhumiwa amekutwa na hatia kutokana na ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo, awali Mwendesha Mashtaka wa Serikali Veneranda Masai aliiomba Mahakama kutoa adhabu Kali kutokana na kitendo kilichofanyika kimemuathiri Mtoto huyo.

Aidha Mahakama ilimpa nafasi ya kujitetea ambapo Mtuhumiwa aliiomba Mahakama kumpunguzia adhabu kwasababu ana Mtoto Mdogo na anamtegemea lakini hata hivyo Mahakama ikamuhukumu kifungo cha maisha kwa kosa la kumlawiti Mtoto huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live