Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Avamia klabu ya wapenzi wa jinsia moja na kuua watano

Mklg Avamia klabu ya wapenzi wa jinsia moja na kuua watano

Sun, 20 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takriban watu watano wameuawa na wengine 18 kujeruhiwa baada ya mtu mwenye silaha kushambulia kwa risasi klabu ya wapenzi wa jinsia moja katika jimbo la Colorado nchini Marekani Jumamosi usiku.

Polisi walisema mshukiwa, kwa jina Anderson Lee Aldrich, 22, amekamatwa na anatibiwa majeraha.

Watu wawili "mashujaa" kwenye kilabu walifanikiwa kumdhibiti mshambuliaji, polisi walisema.

Club Q, huko Colorado Springs, ilitoa taarifa kwenye Facebook ikisema "imehudhunishwa na shambulio lisilo na maana kwa jamii yetu".

Polisi wa Colorado Springs waliwataka watu kuwa na subira wakati wanafanya kazi ya kutambua waathiriwa na kukamilisha idadi ya majeruhi. Mshukiwa huyo alipatikana ndani ya klabu hiyo wakati polisi walipoingia.

Mwaka wa 2016, watu 49 waliuawa na zaidi ya 50 kujeruhiwa kwa risasi kwenye klabu ya usiku ya wapenzi wa jinsia moja huko Orlando, Florida. Kwa wakati huo hayo yalikuwa mauaji mabaya zaidi ya watu wengi kwa wakati mmoja katika historia ya Marekani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live