Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Auawa na rafiki yake kisa simu

Kifo Kifo Mauiaji.png Auawa na rafiki yake kisa simu

Wed, 24 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana Shaban Athuman Mgosi (39) mkazi wa Majengo Mapya mjini Moshi ameuawa leo Aprili 24, 2024 majira ya saa 12:20 asubuhi baada ya ugomvi baina yake na rafiki yake kuhusu masuala ya simu.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema siku za hivi karibuni walikuwa wakivutana na rafiki yake kuhusu simu ambapo asubuhi ya leo alimwamsha kama anataka kuzungumza naye ndipo alipomkata na kitu chenye ncha kali maeneo ya shingo na kijana huyo kufariki papo hapo.

Mtuhumiwa wa mauaji hayo anayefahamika kwa jina la Rajabu amekimbia kusikojulikana ambapo katika chumba cha mtuhumiwa ilionekana simu ikiwa imetapakaa damu.

Mwenyekiti wa Mtaa huo Bi Kimambo amethibitisha kuwapigia simu Polisi ambao walifika mara moja eneo la tukio na kuubeba mwili wa marehemu kwa hatua zaidi za uchunguzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live