Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Auawa kwa wivu wa mapenzi

Wivu Pc Data Auawa kwa wivu wa mapenzi

Wed, 5 Jan 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Mlinzi katika kiwanda Cha Machapati, Juma Mgunda,75,ameuawa kwa kupigwa shoka kichwani na mgongoni akiwa chumbani kwake.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema kuwa tukio hilo limetokea  Januari 4 katika Mtaa wa Kachoma,wilayani Nzega.

Amesema siku ya tukio,akiwa chumbani kwake,mlinzi huyo anadaiwa kufuatwa na Juma Lyamba ambaye anatuhumiwa kumpiga kwa kutumia shoka eneo la kichwani na mgongoni na kusababisha kifo chake.

Amesema mtuhumiwa alikuwa anamtuhumu mlinzi huyo kwa kushirikiana na mganga wa kienyeji anayejulikana kwa jina moja la James,kumtorosha mke wake aitwaye Hadija Nyahindi.

"Chanzo Cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi kwani mtuhumiwa alimtuhumu marehemu na mganga wa kienyeji kumtorosha mkewe kwa muda wa mwezi mmoja Sasa"Amesema

Kamanda Abwao amesema mtuhumiwa alikamatwa akiwa na shoka linalodaiwa kutumiwa kufanya mauaji hayo baada ya wananchi kutoa taarifa kutokana na tukio hilo.

Advertisement Amesema mtuhumiwa amekamatwa na kuwa upelelezi wa tukio hilo unaendelea na mara utakapokamilika,atafikishwa mahakamani.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz