Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Auawa kwa risasi kisa chipsi

Bastola Cjhipsi Auawa kwa risasi kisa chipsi

Mon, 8 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bado mauaji ya risasi yanazidi kuwa pasua kichwa nchini Marekani ambapo tukio jipya linahusu Mfanyakazi wa mgahawa wa McDonald mwenye umri wa miaka 23 kupigwa risasi shingoni wakati wa ugomvi kuhusu chakula Brooklyn, New York.

Polisi wamesema Mteja Mwanamke mwenye umri wa miaka 40 alilalamika kuwa amepewa chipsi za baridi na hapo ndipo mabishano yalianza hadi kumpigia simu Mtoto wake wa kiume kupitia facetime ambaye alifika kwenye mgahawa huo kwa haraka.

Polisi wanasema kijana huyo wa miaka 20 alimuita Mfanyakazi huyo nje kisha akatoa bunduki na kumpiga risasi shingoni ambapo pamoja na kwamba aliwaishwa Hospitali… alifariki siku mbili baadaye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live