Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Auawa kwa madai ya kuiba korosho kilo 10

RPC Mtwara Auawa kwa madai ya kuiba korosho kilo 10

Wed, 26 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi Mkoani Mtwara wamesema wanafanya uchunguzi wa tukio la mauaji yaliyotokea October 21,2022 katika Kijiji cha Mbawala chini Mkoani wa Mtwara ambapo Waziri Mnyelema (21), Mkazi wa Kijiji cha Mkangala alifariki dunia baada ya kupigwa mawe na magongo ya miti kwa tuhuma za kuvunja nyumba na kuiba korosho kilo 10.

“Siku ya tukio Waziri alifika nyumbani kwa Casto Salumu ambapo hapakuwa na Mtu na kuvunja mlango wa nyumba kisha kuiba korosho kilo 10, radio, mto wa kulalia na betri ndogo ya solar.

“Tukio hilo la kuvunja nyumba lilishuhudiwa na baadhi ya Wananchi ambapo walianza kuhamasishana kwa kelele za ‘Mwizi Mwizi’ kisha walimkamata Mtu huyo aliyekuwa akikimbia na mali hizo hatimaye walimshambulia kwa kutumia mawe na magongo na kufariki Dunia.

“Uchunguzi wa kitabibu umebaini sababu ya kifo ni Kuvuja damu kwa wingi kutokana na majeraha makubwa kichwani na sehemu mbalimbali za mwill wake, aidha juhudi zinafanyika kuweza kuwakamata Watu wote waliohusika katika tukio hili ili wafikishwe mbele ya sheria.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live