Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Auawa kwa fumanizi

64187 FUMANIZI+PIC

Tue, 25 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Shinyanga. Watu watano wameuawa katika matukio tofauti mkoani hapa likiwamo la mwanaume aliyeuawa baada ya kufumaniwa na mke wa mtu.

Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, Richard Abwao alisema tukio hilo lilitokea Juni 21 kitongoji cha Mwasele B mji mdogo wa Mhunze wilayani Kishapu, Shija Mahohiga (45) aliuawa baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa mtu ndani ya nyumba.

Abwao alimtaja mtuhumiwa anayeshikiliwa kuwa ni mkazi wa Mhunze ambaye ni mume wa mwanamke huyo, Maria Kija. Pia, katika purukushani hizo, Maria alijeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Jakaya wilayani Kishapu.

Katika matukio mengine yaliyotokea ni mauaji ya mkeNyamizi Mserengeti (40) na muwewe Manyara Nderema (48) wakazi wa Masengwa wilayani Shinyanga, waliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni wakiwa wamelala.

Chanzo cha mauaji hayo yaliyotokea Juni mosi ni ugomvi wa familia kuhusu mashamba yanayomilikiwa na Nderemo ambayo aliyanunua kutoka familia yao, watuhumiwa sita wanashikiliwa na polisi.

Tukio jingine ni mauaji yaliyotokea Juni 7 kijiji cha Busangi wilayani Kahama baada ya kuvamiwa na kukatwa mapanga kwa Zainab Shija (28), chanzo kikitajwa ni wivu wa mapenzi.

Pia Soma

Mauaji mengine yalifanyika eneo la Kitangili Juni 19, Ester Samwel (35) mkazi wa Ndembezi aliuawa kwa kupigwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili na wananchi akidaiwa kuiba debe la nyanya soko la Kitangili.

Kamanda Abwao alisema msako wa waliohusika unaendelea.

Chanzo: mwananchi.co.tz