Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Auawa kisa ‘chenji’ ya sigara

Hand In Cuffs Auawa kisa ‘chenji’ ya sigara

Tue, 7 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

POLISI katika Jimbo la Ogun wanamshikilia mwanaume aliyefahamika kwa jina la Biodun Adebiyi kwa kosa la kumuua mwenzake wakati anadai ‘chenji’ ya sigara dukani.

Siku ya tukio, Jumapili ya wiki iliyopita, Adebiyi mwenye umri wa miaka 32, mkazi wa Ikotum, Lagos, alinunua sigara dukani kwa Mukaila Adamu (30) na kisha kuondoka zake.

Baadaye, mtuhumiwa huyo alirudi na kuanza kudai chenji yake, Naira 50 (Sh. 270 za Tanzania), jambo ambalo Adamu hakukubaliana nalo akiamini alishamaliza naye.

Tofauti hiyo ilizua zogo kati yao na kwa mujibu wa baba yake Adam, mtoto wake alianguka chini baada ya Adebiyi kumpiga ngumi.

Hiyo ilisababisha akambizwe hospitali, jitihada ambazo hata ziliishia kwa muuzaji duka huyo kupoteza maisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live