Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Auawa baada ya kuiba mahindi

Auawa Baada Ya Kuiba Mahindi Auawa baada ya kuiba mahindi

Thu, 12 Jan 2023 Chanzo: Radio Jambo

Umati wenye hasira katika lokesheni ndogo ya Bonyaiguba, Kaunti ya Nyamira wamemuua mwanamume waliyemshutumu kwa kuiba mahindi kutoka kwa shamba la jirani.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Nyamira, Moses Kirong alithibitisha kisa hicho akisema James Ondigo mwenye umri wa miaka 28, alipatikana akiwa na mahindi yanayoaminika kuibwa kutoka shamba moja katika kijiji cha Engoto mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi kabla ya umati huo kumpiga hadi kumuua. .

Alisema msaidizi wa chifu wa Bonyaiguba, Joseph Obiero, ambaye aliripoti kisa hicho alisema raia wenye ghadhabu walimvamia marehemu ambaye walimpiga kwa mawe hadi akakata roho.

"Walimpiga kwa mawe hadi akafariki dunia wakati maafisa walipofika eneo la tukio" alieleza Kirong.

"Tulikuwa na taarifa za awali kwamba marehemu alijulikana kwa vitendo vya wizi mdogo kijijini lakini tunalaani vikali wale wanaojihusisha na kuchukua sheria mkono lakini tuna vyombo vya sheria ambavyo vingeweza kumshughulikia kisheria." Alisema.

Mwili wa James, uliokuwa na majeraha mengi yanayoonekana, ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya rufaa ya kaunti ya Nyamira ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.

Chanzo: Radio Jambo