Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Auawa akidai Sh6, 500

Polisi Pic Mzaaaa Auawa akidai Sh6, 500

Fri, 26 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Kata ya Nyakabungo Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Peter Domini (48) ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani alipokwenda nyumbani kwa Julius Gaini (59) kudai Sh6,500 ya malipo ya pombe aliyomkopesha kilabuni kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 26, 2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amesema tayari wanawashikilia watu watatu wa familia moja wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo lililotokea Mei 25 mwaka huu Saa 2 usiku.

“Peter Domini alifika nyumbani kwa Julius Gaini (59) mkazi wa Nyakabungo kwa nia ya kudai pesa yake Sh6,500 na baada ya kufika ulizuka ugomvi baina yao na kupelekea marehemu kushambuliwa,”

“Baada ya tukio hilo jeshi la polisi limefanya ufuatiliaji wa tukio hilo na kuwakamata Julius Gaini, Judith John (48) na Roda Julius (49) wakazi wa Nyakabungo kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Peter Domini, upelelezi katika tukio hili unaendelea na watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika,” amesema

Katika tukio lingine, jeshi hilo linawashikilia waganga wakienyeji 33 kwa madai ya kujihusisha na upigaji ramli chonganishi na kufanya shughuli za uganga wa kienyeji bila kufuata taratibu za kisheria.

Mutafungwa amesema katika oparesheni hiyo iliyofanyika kuanzia Mei 17 hadi 25, 2023 wamefanikiwa kukamata vielelezo mbalimbali ambavyo huvitumia kwenye shughuli zao.

“Nitoe wito kwa waganga wote wa kienyeji ambao wanafanya shughuliz hizo wafike katika ofisi za utamaduni ili kupata vibali vya kufanya shughuli hizo ili kupunguza matukio ya uharifu ambayo husababishwa na imani potofu,”amesema Mutafungwa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live