Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aua wanawe, amjeruhi mkewe kisha ajinyonga

17492 AJOIUA+PIC TanzaniaWeb

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Dotus Isaya, mkazi wa Chanika jijini Dar es Salaam amewaua watoto wake wawili na kumjeruhi mkewe, Mariam Lucas na kisha kujinyonga hadi kufa.

Dotus amefanya kitendo hicho cha kusikitisha usiku wa kuamkia leo wilayani Nachingwea mkoa wa Lindi.

 

Akizungumza na MCL Digital leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Pudensiana Protasi alisema Dotus alikwenda Lindi anakoishi mkewe na kufanya tukio hilo la kinyama.

 

Alisema kabla ya kutekeleza mauaji hayo marehemu alikuwa na ugomvi na mkewe na baada ya muda mfupi alimkata kwa panga kichwani na begani.

 

“Baada ya kumkata mkewe alikwenda chumba wanacholala watoto wake na kulikuwa na watoto wanne lakini aliwakata mapanga wanawe tu,” alisema.

 

Kamanda Pudenciana aliwataja watoto hao kuwa Clara Dotus (5) na Erieth Dotus (3) na baada ya kufanya mauaji hayo alikwenda katika chumba cha mkewe na kujinyonga kwa kutumia khanga.

 

Alisema Mariam amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea.

Chanzo: mwananchi.co.tz