Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aua mkewe akimtuhumu kumwibia na kufungua duka

Crimeee Aua mkewe akimtuhumu kumwibia na kufungua duka

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi nchini Kenya linamshikilia Boniface Kokwon mwenye umri wa makamo kwa tuhuma za kumsambulia mkewe Ivy Chelagat kwa mawe hadi kumuua.

Kwa mujibu wa Tuko News na Jambo Radio za nchini humo, tukio hilo limetoka Jumamosi Machi 9, 2024 ambapo mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo huku chanzo kikielezwa kuwa alimshuku kumwibia fedha dukani na kufungua la kwake, katika eneo la Biretwo, Kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Inaaminika Chelagat alifungua duka lake umbali wa mita 100 kutoka kwenye duka la mumewe.

Siku ya tukio, Kokwon alienda akamtoa mkewe nje kisha akampeleka pembeni na kuanza kumshambulia kwa mawe.

Walioshuhudia wamesema waliukuta mwili wa marehemu ukiwa umelala chini huku mumewe akiwa ameshikilia kisu na pembeni kukiwa na jiwe linalodaiwa kutumika kumuulia Chelagat.

Kokwon ambaye ni mfanyabiashara alikamatwa na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Iten, ambako anazuiliwa akisubiri kufikishwa mahakamani.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Iten.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live