Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aua mke, ajinyonga kwa kilemba

Ajinyonga Hsgd Aua mke, ajinyonga kwa kilemba

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rashidi Hussein Mkayaga mkazi wa Mtaa Gemu, Kata ya Mwanga Kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji, amejinyonga kwa kutumia kilemba cha kiume cha kuvaa kichwani, muda mfupi baada ya kumuua mke wake Bernadeta Cosmas kwa kumnyonga shingo hadi kufa kwa kile kinachodaiwa ni mgogoro baina ya wanandoa hao.

Mwenyekiti wa Mtaa Gemu, Buswalu Mkama akizungumzia na waandishi wa habari eneo la tukio, amedai chanzo ni mgogoro wa muda mrefu na kwamba mwanamke huyo aliwahi kufika kwake na kutoa malalamiko ya vitendo vya mume wake kuchukua vitu vya ndani na kuuza na mara kadhaa kesi hizo alizisuluhisha.

Uchunguzi wa awali wa tukio hilo unaonesha kuwa Rashidi Hussein alimnyonga mke wake kwa mikono hadi kumuua na baadaye kutoka nje, ambapo alifunga mlango kwa nje na kurudi ndani kupitia dirishani, ambapo alifunga milango yote na madirisha na yeye kujinyonga kwa kitambaa cha kichwani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live