Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atupwa jela miezi sita kwa kuharibu miundombinu ya maji Dodoma

Hukumu Pc Data Atupwa jela miezi sita kwa kuharibu miundombinu ya maji Dodoma

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: mwanachidigital

Mahakama ya Mwanzo Chamwino Mjini, Mkoa wa Dodoma imemuhukumu, Enock Mwalimu kwenda jela miezi sita kwa kosa la kuharibu miundombinu ya maji kinyume na sheria.

Miundombinu hiyo ni ya Mamkala ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) aliyotuhumiwa kuiharibu Januari 19, 2023, maeneo ya Chang’ombe jijini humo.

Mwalimu alikamatwa saa tatu asubuhi akiwa anafanya ufundi kinyume na taratibu za DUWASA na kufunguliwa kesi ya jinai namba 67/2023.

Akisoma hukumu hiyo jana Alhamisi, Februari 16, 2023, Hakimu Mkazi, Raymond Kweka alisema mshtakiwa alikiri kosa na alipohojiwa kuhusu tukio hilo alisema alikuwa anarekebisha bomba.

Hakimu alisema, mshtakiwa alipoulizwa alisema alikuwa tayari ameshakatakata mabomba na kuinyofoa mita ya maji na hakusema alitaka kuipeleka wapi.

“Mahakama lazima ijiridhishe pasipo kuacha shaka yeyote kuwa mshtakiwa ametenda kosa na katika shauri hili mshatkiwa hakuona sababu ya kuisumbua mahakama kwani alikubali kutenda kosa aliloshtakiwa nalo katika hati ya shtaka,” alisema Hakimu Kweka

Hivyo kwa msingi huo wa kisheria Mahakama ya Mwanzo imemtia hatiani mshtakiwa chini ya kanuni ya 37 (1) cha jedwali la tatu la sheria ya Mahakama za mahakimu sura ya 11 mapitio ya waka 2019 kosa moja la kuharibu mali kinyume cha sheria.

Mtuhumiwa aliomba kupunguziwa adhabu kwa sababu anafamilia inayomtegemea na yeye ndio kila kitu katika familia pia ni kosa lake la kwanza.

“Kwakuwa mshtakiwa ametenda kosa hili kwa mara ya kwanza, kuzingatia maombi yake Mahakama imeamuru atumikie kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini,” alisema Hakimu Kwema

Hakimu Kweka amesema rufaa ipo wazi kwa siku 30 kama kuna atakayeona hajatendewa haki.

Chanzo: mwanachidigital