Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atupwa jela miaka miwili kwa kukutwa na nyama ya Pofu

Pofu Pofu Atupwa jela miaka miwili kwa kukutwa na nyama ya Pofu

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAHAKAMA ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma imemuhukumu kifungo cha miaka miwili jela Ally Rashidi Mbalamla (30), Mkazi na Kijiji cha Muhuwesi Wilaya ya Tunduru, baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na nyara za serikali.

Akisoma hukumu ya kesi ya Jinai Na.7964 ya mwaka 2024, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Lilian Haule amesema mahakama imefikia uamuzi huo, baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo kuacha shaka yoyote.

Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Desemba 01, 2023 kwa kukutwa na vipande 14 vya nyama ya pofu katika Kijiji cha Muhuwesi na kufikishwa mahakamani Machi 25, 2023 na siku hiyo hukumu kutolewa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live