Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atupwa jela miaka 60 kwa kumbaka na kumpa ujauzito mwanaye

Jela Miaka 30 Atupwa jela miaka 60 kwa kumbaka na kumpa ujauzito mwanaye

Fri, 28 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Ubungo, Makoka, jijini Dar es Salaam, William Mwangweo amehukumiwa kifungo cha miaka 60 jela baada ya kukiri kosa la kubaka na kumpa ujauzito mtoto wake wa miaka 16 aliposhawishiwa na rafiki yake anywe dawa kwa ajili ya kuvutia wateja kwenye bodaboda yake.

Mshtakiwa huyo alikiri kosa la kumbaka mwanaye na kumpa ujauzito mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Yusuph Makamba baada ya Mahakama hiyo kumkumbusha makosa yake.

Hukumu hiyo imetolewa jana Alhamisi Oktoba 27, 2022 na Hakimu Mwandamizi, Amos Rwekiza baada ya mshtakiwa huyo kukiri makosa yote mawili la kubaka na la kumpa ujauzito binti yake.

Hakimu Rwekiza amesema kwa kuwa mshtakiwa huyo amekiri kufanya mapenzi na mwanaye ameenda kinyume kifungu cha 158(1) cha Sheria ya makosa ya jinai sura namba 16 ya marejeo ya mwaka 2019.

Kosa la kumpa ujauzito binti yake ambaye ni mwanafunzi ameenda kinyume na kifungu cha 60A(3) cha Sheria ya elimu mamba 353 marejeo ya mwaka 2002 hivyo mahakama hiyo  imemtia hatiani kwa makosa yote mawili.

Amesema mahakama hiyo inamuhukumu mshtakiwa huyo kwenda jela miaka 40 kwa kosa la kubaka mwanaye na kosa la kumpa ujauzito mwanafunzi anahukumiwa kwenda jela miaka 20.

"Kosa la kwanza la kubaka atatumikia miaka 40 jela na la pili la kumpa ujauzito binti yake atatumikia  miaka 20 jela jumla atatumikia miaka 60 jela," amesema Rwekiza.

Hakimu Rwekiza  ilipomtaka mshtakiwa huyo ajitetee mbele ya mahakama hiyo alidai alimbaka na kumpa mimba binti yake hivyo hakutaka kuisumbua mahakama hiyo

Mshtakiwa huyo alidai yeye ni dereva wa bodaboda alikuwa na maisha magumu ndipo rafiki yake alimpa dawa aweze kupata wateja wengi.

Alidai wakati anaendelea kunywa dawa hizo alizopewa na rafiki yake  bika ya kutegemea alianza kumtamani  kimapenzi binti yake.

Mshtakiwa huyo alidai maisha yake yaliendelea kuwa magumu ndipo binti yake alimshawishi wafanye mapenzi ili baba yake aweze kupata wateja wengi kwenye bodaboda aliyokuwa akiendesha

"Naomba mahakama hui inipunguzie adhabu kwa kuwa anajutia kosa lake ana watoto 10 wanaomtegemea hawezi kurudia tena kufanya hivyo kwa kuwa alidanganywa na rafiki yake atumie dawa kwa ajili ya kuvutia wateja kwenye bodaboda yake,"alidai mshtakiwa Mwangweo.

Awali, wakili WA serikali Chessensi Gavyole aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu Kali ili iwefundisho kwa webye tabia kama hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live