Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atupwa jela miaka 22 kwa kukutwa na vichwa vitano vya pundamilia

ZEBR Pundamilia Atupwa jela miaka 22 kwa kukutwa na vichwa vitano vya pundamilia

Thu, 13 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Babati mkoani Manyara imemuhukumu Silvesta Irusu (51) mkazi wa Sangaiwe kifungo cha miaka 22 kwenda jela kwa kosa la kukutwa na vichwa vitano vya pundamilia pamoja na nyama ambazo ni nyara za Serikali.

Mwendesha mashtaka wa Serikali Grace Mgaya, amesema mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 28, 2021 katika hifadhi ya Burunge akiwa na wenzake ambao walifanikiwa kukimbia lakini yeye aliweza kuanguka na kukamatwa na kukutwa na vichwa vitano vya punda milia, mikia mitano, kwato ishirini pamoja na nyama ambayo thamani yake ni zaidi ya Sh. Milioni 13 sawa na punda wa tano.

Mgaya ameiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa kuwa mshtakiwa sio mara ya kwanza kushtakiwa kwa makosa hayo ambapo aliwahi kuhukumiwa miaka 30 jela kabla ya hukumu ya jana.

Mshtakiwa ameiomba Mahakama hiyo iweze kumpunguzia adhabu kwakuwa ana watoto saba pamoja na Mama yake mzazi ambae ni Mzee na wote wanamtegemea.

Hakimu wa Mahakama hiyo ya Wilaya Victor Kimario amemuhukumu kwenda jela miaka 22 huku haki ya kukata rufaa ikiwepo ndani ya siku 30 kuanzia jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live