Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atupwa jela maisha kwa kuua watu 6, na kuwajeruhi 62

Marekani Web Atupwa jela maisha kwa kuua watu 6, na kuwajeruhi 62

Fri, 18 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jaji mmoja wa Wisconsin amemhukumu mtu aliyewaua watu sita na kuwajeruhi 62 kwa kuendesha gari kupitia gwaride la Krismasi mwaka jana kwenda jela maisha.

Jopo la majaji lilimtia hatiani Darrell Brooks mwezi uliopita baada ya waendesha mashtaka kudai kuwa alionyesha "kutojali kabisa maisha ya binadamu".

Mahakama pia ilisikiliza ushahidi wa kutoka kwa mashahidi waliokua na hisia kali ambao ni makumi ya manusura na familia za waathiriwa wakati wa hukumu. Brooks alijiwakilisha mwenyewe katika kesi hiyo ya wiki nne.

Katika hukumu yake siku hiyo Jaji Jennifer Dorow alisema Brooks alichagua "njia ya uovu".

Alimwamuru kutumikia kifungo cha maisha sita  kimoja kwa kila mwathiriwa wa mauaji , na kwa mfano aliongeza kifungo kingine cha miaka 1,067 jela kwa makosa yake mengine.

Mauaji hayo yalifanyika katika gwaride la Krismasi la kila mwaka katika mji wa Waukesha mnamo Novemba 21, 2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live