Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atupwa jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka nane

Wnanaume Saba Rape Atupwa jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka nane

Thu, 28 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa, imemhukumu Kelvin Mkung'a (23), Mkazi wa Mgololo kifungo cha maisha jela, baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka nane.

Akizungumza jana Jumatano, Julai 27, 2022, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Sekela Kyungu alisema mshtakiwa huyo alimbaka mtoto huyo Januari 3, 2022 katika kijiji cha Kitasengwa Kata ya Makungu tarafa ya kasanga wilayani humo.

Alisema kesi hiyo ya Jinai namba 1 ya mwaka 2022 ambapo Mahakama imemtia hatiani na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela kutokana na mshtakiwa kutenda kosa hilo.

"Mshtakiwa anatuhumiwa kwa kosa la ubakaji ambayo in kinyume na kifungu namba 130 (1) (2)(e) na kifungu 131(3) cha sheria ya kanunu ya adhabu sura ya 16 rejeo la mwaka 2022 baada ya upande mashtaka kudhibitisha kosa hilo kwa mshatakiwa bila kuacha shaka," alisema  Kyungu

Aidha, Kyungu alisema mahakama hiyo imemtia hatiani mshatakiwa huyo kwa kosa la kubaka na hivyo kupewa adhabu hiyo ya kifungu cha maisha jela kwa mujibu wa kifungu namba 131(3) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 rejeo la mwaka 2022.

Kyungu alisema adhabu hiyo imetolewa Julai 25, 2022 mahakamani hapo ili iwe fundisho kwa mshatakiwa pamoja na jamii nzima kuhusiana na matukio hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live