Fri, 17 Feb 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mahakama ya Wilaya ya Arusha, imemhukumu kifungo cha maisha gerezani, Kelvin Laizer (19) baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka nane.
Laizer ambaye ni mkazi wa eneo la Muriet jijini Arusha amehukumiwa leo Ijumaa, Februari 17,2023 na Hakimu Mkazi Pamela Meena baada ya kumtia hatiani kwa kosa hilo la kumbaka mtoto huyo kwa nyakati tofauti.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu huyo amesema mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa huyo aliyekuwa anakabiliwa na kosa la ubakaji kinyume na kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live