Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atupwa jela maisha kwa kulawiti mtoto

10461 JELA.png TanzaniaWeb

Sun, 1 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Pangani. Mahakama ya Wilaya ya Pangani imemhukumu Chacha Matiku (29) kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa kiume wa kaka yake mwenye miaka tisa licha ya kujitetea kwamba hana nguvu za kiume.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na hakimu mfawidhi mkazi wa Mahakama hiyo, Joel Mnguto baada ya kusikiliza ushahidi na maelezo ya pande zote mbili.

Hakimu Mnguto alisema Mahakama imeridhika na ushahidi pamoja na maelezo yaliyotolewa na upande wa mashtaka na kubaini kwamba Matiku alitenda kosa hilo bila shaka yoyote.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka wa Jeshi la Polisi, Kopro Seif Makono mbele ya hakimu Mnguto kuwa Septemba 12, 2017 saa 6.30 usiku katika Kijiji cha Kasanga, wilayani Pangani, mshtakiwa alimlawiti mtoto huyo (jina limehifadhiwa) huku akijua kufanya hivyo ni kosa.

Kesi hiyo iliendeshwa kwa upande wa mashtaka kupeleka mahakamani mashahidi watano akiwamo mtoto aliyelawitiwa huku upande wa utetezi ukikosa shahidi.

Alipotakiwa kujitetea baada ya kupatikana na hatia, Matiku alimweleza hakimu kwamba asingeweza kutenda kosa hilo kwa sababu hana nguvu za kiume.

“Mheshimiwa hakimu, nashangaa hawa watu wamenileta huku na kudai nimelawiti...hivi mtu asiyekuwa na nguvu za kiume anaweza kufanya jambo kama hilo?” mshtakiwa huyo alimhoji hakimu na kusababisha watu waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo pamoja na hakimu mwenyewe kuangua kicheko.

Hata hivyo, utetezi huo haukumsaidia mshtakiwa kwa kuwa hakimu Mnguto alisema anamhukumu kifungo cha maisha kwa sababu tayari amemwathiri mtoto huyo kisaikolojia na kuharibu maisha yake.

Chanzo: mwananchi.co.tz