Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atupwa jela kwa kuwashtua kuku wa jirani mpaka kufa

Kuku Er.jpeg Kuku

Mon, 10 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamume mmoja nchini China amefungwa jela miezi 6 kwa kuwashtua kuku wa jirani hadi kufa.

Katika kesi ya udadisi iliyoripotiwa katika vyombo vya habari vya serikali ya nchi hiyo, mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la kwanza la Gu alihukumiwa kifungo jela wiki hii baada ya mahakama kumkuta na hatia ya kuwatisha kuku 1,100 wa jirani ambaye alikuwa na ugomvi naye. Kuku hao wote walikufa kutokana na kutishwa huko.

Wawili hao waliripotiwa kugombana tangu jirani, Zhong, kukata miti ya Gu bila ruhusa mnamo Aprili 2022, CNN waliripoti.

Mahakama katika kaunti nchini China ilisikia kwamba Gu alijibu kwa kujipenyeza kwenye shamba la kuku la Zhong wakati wa usiku kwa zaidi ya mara moja akifanya majaribio ya kuwatisha kuku wake.

Haijulikani nia ya Gu ilikuwa ni nini lakini tochi aliyotumia ilisababisha kundi la kuku kuingiwa na hofu na huku ndege hao wakijaa kwenye kona kwa hofu, mamia yao walikufa katika kisanga kilichofuata.

Mara ya kwanza Gu alipovamia mali ya jirani yake, alisababisha mshtuko ambapo kuku 500 walikufa. Alikamatwa na polisi na kulazimishwa kulipa fidia ya Zhong ya $436 sawa na shilingi elfu 58 za Kenya.

Lakini hakuishia hapo na akarudi katika mali ya Zhong mara ya pili, wakati huu akiwaua kuku 640.

Siku ya Jumanne, mahakama ya Hengyang iliamua kwamba Gu alikuwa amesababisha "hasara ya mali" kwa Zhong kimakusudi.

Mamlaka ya Uchina ilisema kuwa kuku hao 1,100 waliokufa walikadiriwa kuwa na thamani ya jumla ya $2,015 sawa na shilingi elfu 266 za Kenya.

Mahakama iliamuru Gu kutumikia kifungo cha miezi sita gerezani na mwaka mmoja wa majaribio - hukumu ambayo ilisema ilizingatia majuto ambayo Gu alikuwa ameonyesha kwa uhalifu wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live