Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atupwa Jela miaka 5 kwa kuvunja nyumba na kuiba Debe la Maharage

WhatsApp Image 2022 05 14 At 12.jpeg Atupwa Jela miaka 5 kwa kuvunja nyumba na kuiba Debe la Maharage

Sun, 15 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya mwanzo ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imemhukumu Ombeni Ngwa’vi (25) kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kuvunja nyumba ya Evaristo Mgimba pamoja na miaka mingine miwili kwa kuiba debe moja la maharage ambapo vifungo hivyo vitaenda kwa kufuatana.

Akisomewa shitaka hilo Mwendesha mashtaka Asifiwe Asajile mbele ya hakimu Timoth Mwakisambwe imedaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Mei 12 mwaka huu majira ya mchana ambapo alivunja nyumba ya Evaristo Mgimba kisha kuiba debe moja la maharage lenye thamani ya shilingi 30,000.

Mtuhumiwa huyo amekiri kutenda kosa hilo ikiwa ni kinyume na kifungu cha sheria namba 294(1)(a), 258(1) na 265 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya 2019.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live