Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atupwa Jela miaka 30 kwa kumbaka Mwanafunzi wa darasa la 4

Nyundoo Atupwa Jela miaka 30 kwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la 4

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha miaka 30 Petro Mgimwa aliyekuwa akiishi katika Kijiji cha Ifunda kwa kosa la kubaka Mtoto mwenye umri wa miaka 9 aliyekuwa akisoma darasa la nne.

Petro (41) alikuwa akifanya kazi ya ulinzi na ukulima ambapo alimrubuni Mtoto huyo kwa kumpa maembe na baada ya kumaliza kumbaka akampa Tsh. Elfu 1.

Kwa Mujibu wa Mahakama tukio hilo lilitokea March 06,2022 ambapo Binti alikwenda kuchuma maembe katika nyumba ambayo Petro alikuwa akilinda ndipo Petro akamrubuni na kumuingiza ndani ya chumba Kisha kumbaka.

Baada ya kumaliza Binti alipokwenda nyumbani Dada yake alimgundua kwa sababu alikuwa anatembea tofauti na alivyomzoea ndipo akamhoji na akaambiwa kuwa alikuwa amebakwa.

Kesi hiyo iliyosimamiwa na Mwendesha mashtaka wa Serikali Penzia Nochombe ilikuwa na Mashahidi 6 akiwemo Daktari aliyemfanyia uchunguzi Binti huyo na kubaini kuwa alikuwa amebakwa, akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu Zabibu Mpangule amesema Mtuhumiwa amekutwa na hatia kutokana na mashahidi wote kumthibitisha kuwa Petro Mgimwa alimbaka Mtoto huyo na hivyo amehukumiwa miaka 30 Jela.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live