Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atuhumiwa kutumia jina la Makamba vibaya

18017 Pic+makamba TanzaniaWeb

Wed, 19 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam, Ahmed Mohamed amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kujibu mashtaka matatu likiwamo la kujitambulisha kwa nia ovu kuwa yeye ni Mwamvita Makamba.

Mwamvita ni dada yake, January Makamba ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Wakili wa Serikali Neema Kiliwa, amesoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Karoline Kiliwa leo Septemba 18,2018, akidai katika shtaka la kwanza Julai 6, 2018 eneo la White Sand alimbaka mtoto na kumsababishia maumivu makali sehemu mbalimbali ya mwili wake.

Katika shtaka la pili amedai tarehe tofauti kati ya Juni 17 hadi Julai 7,2018 katika Jiji la Dar es Salaam Mohamed alijitambulisha yeye ni Mwamvita Makamba kupitia namba ya simu ya mkononi 0787239647 kwa nia ovu wakati akijua kufanya hivyo ni kosa. 

Katika shtaka la tatu mtuhumiwa huyo kwa tarehe tofauti kati June 18 hadi Julai 7,2018 katika jiji la Dar es Salaam alijitambulisha yeye anaitwa  Edd ni  wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kupitia namba ya simu ya mkononi 0624603817 huku akijua kufanya hivyo ni kosa.

Baada ya maelezo hayo mtuhumiwa alikana kutenda makosa yote matatu yanayomkabili ambapo wakili amedai upelelezi bado hujakamilia . 

Hakimu Kiliwa  amesema dhamana ipo wazi awe na wadhamini wawili wenye barua za utambuzi  wa sehemu wanazofanyia kazi.

Mtuhumiwa alirudishwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti hayo hivyo kesi imeahirishwa  hadi Oktoba 2, 2018.

Chanzo: mwananchi.co.tz