Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atuhumiwa kuiba Milioni 19 kwenye Kibubu

RPC Wa Manyara George Katabazi.jpeg RPC wa Manyara George Katabazi

Wed, 21 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana Gift Fredrick (22) Mkazi wa Mirerani anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara kwa kukutwa na fedha za wizi kiasi cha Tsh. milioni 19, fedha ambazo zilihifadhiwa kwenye Kibubu na Mfanyabiashara Isaya Philipo (29).

RPC wa Manyara George Katabazi amesema tukio hilo limetokea June 18, 2023 huko katika Mtaa wa Kangaroo Kata ya Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

Mfanyabiashara huyo Isaya Philipo alikuwa akihifadhi fedha hizo nyumbani kwake kwenye sanduku la chuma(kibubu) ambapo Mtuhumiwa alipata taarifa na kuiba sanduku hilo “Fedha hizo zimehifadhiwa kituo cha Polisi Mirerani kama kielelezo na Mtuhumiwa anahojiwa ili kujua anaoshirikiana nao"

Hii inakuwa ni mara ya tatu katika kipindi cha miezi miwili kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara kufanikisha kukamata fedha zinazoibiwa kwa Wananchi pamoja na Wahalifu wa matukio hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live