Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atuhumiwa kubaka watoto 15 akidai ni askari polisi

Allan Bukumbi Srf Atuhumiwa kubaka watoto 15 akidai ni askari polisi

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Alex Msigwa (34) Dereva wa Bajaji, Mkazi wa Mawelewele, Manispaa na Mkoa wa Iringa anashikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma za ubakaji katika maeneo mbalimbali ndani ya Manispaa akiwalubuni WATOTO kwa akijitambulisha kuwa yeye ni Askari polisi wakati mwingine akidai yeye ni Afisa ustawi wa jamii jambo ambalo si la kweli.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP – Allan Bukumbi mbele ya Waandishi wa Habari inaeleza kuwa Mtuhumiwa huyo hadi anakamwatwa alikuwa ameshafanya matukio zaidi ya 15 ndani ya Mkoa huo.

“Mara baada ya kumkamata tuliwaita wazazi kuja na watoto ambao ni wahanga waliweza kumtambua Mtuhumiwa kwani alikuwa anakovu sehemu ya Mdomo wake, wakati tunamuhoji alidai anafanya hivyo kwa tamaa zake tu,” alisema Kamanda Bukumbi.

Aidha Kamanda Bukumbi aliongeza kuwa katika uchunguzi wa awali walioufanya walipo chukua simu ya Mtuhumiwa waliona akiwasiliana na rafiki yake kuwa waende kumbaka kwa kundi (Mande) Mwanamke ambaye hakutajwa jina lake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live