Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atiwa hatiani kwa mauaji ya mwanafunzi wa Scolastica

61137 Pic+hukumu

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, imemtia hatiani mshitakiwa wa kwanza, Hamis Chacha, kwa kosa la kumuua kwa makusudi mwanafunzi wa Scolastica, Humphrey Makundi.

Mbali na kumtia hatiani mshitakiwa wa kwanza, lakini Jaji Firmin Matogolo, amewatia hatiani mmiliki wa shule hiyo, Edward Shayo na mwalimu wa nidhamu, Laban Nabiswa kwa kosa dogo la kushiriki jinai.

Mahakama imeahirishwa kwa dakika 30 hadi saa 8:30 mchana leo Jumatatu Juni 3, 2019 ili kuwawezesha mawakili wa washitakiwa Shayo na Nabiswa waweze kutoa maombolezo yao kabla ya Jaji kutoa adhabu.

Mwanafunzi huyo aliuawa Novemba 6,2017 na baadaye mwili wake kutupwa mto Ghona, mita takribani 300 kutoka shuleni na baadae kuzikwa na Manispaa kabla ya kufukuliwa kwa amri ya mahakama.

Chanzo: mwananchi.co.tz