Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Mwamakula afanya maombi kwa Mbowe na mawakili wake

Maombipic Askofu Mwamakula afanya maombi kwa Mbowe na mawakili wake

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Uamsho Tanzania, Emmaus Mwamakula amefanya maombi kwa mawakili wa upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Mbowe na wenzake wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili vitendo vya kigaidi.

Askofu Mwamakula amefanya maombi hayo, leo Jumatano Oktoba 21, 2021 ndani ya mahakama wazi ilipo katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Askofu huyo amefika mahakamani hapo saa 3:30 na kisha kuingia ndani ya mahakama ya wazi ambapo alikuta watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa Chadema, wafuasi na watu wengine na kisha kuwapungia mkono.

Baada ya hapo alikaa katika eneo ambalo alikuwa ameandaliwa na kisha kuanza kusalimiana na baadhi ya viongozi wa Chadema.

Baada salamu hizo, mawakili wa upande wa utetezi waliosimama na kisha kuombea kwa pamoja huku wakitengeneza duara, kama timu ya mpira ainavyofanyaga sala muda mfupi kabla ya mechi kuanza.

Baada ya sala hiyo, Askofu huyo alirudi kukaa sehemu aliyokuwa amepangiwa.

Ilipofika saa 3:50 asubuhi, Mbowe na wenzake waliingia mahakamani na hapo pia Askofu Mwamakula alinyanyuka na kuwaombea.

Chanzo: mwananchidigital