Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari wa Zimamoto afukuzwa kwa rushwa

50613 Pic+askari

Fri, 5 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Jeshi la Zimamoto na Ukoaji limemfukuza kazi askari mwenye namba US/ZM 2946 FC Joseph Chale kutokana na kuhusika katika vitendo vya rushwa na unyanyasaji kwa wachimbaji wadogo wa madini Wilaya ya Chunya mkoani Songwe.

Pia jeshi hilo limesema wapo maofisa na askari wengine ambao bado shauri lao liko kwenye mahakama za kijeshi kwa utaratibu  na kanuni za jeshi la zimamoto na ukoaji.

Kamishina wa Operesheni Jeshi la Zimamoto na Ukoaji, Billy Mwakatage akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, Aprili 5 jijini hapa amesema askari na maofisa ambao shauri la lipo mahakama ya kijeshi ni US/ZM 3005 A/ INSP Canisium Komba, US/ ZM 3077 A/ INSP Aron Mayunga na US/ ZM 3152 A/ INSP Zawadi Maliga.

“Jeshi la Zimamoto na Ukoaji linatoa taarifa kwa umma kuhusu hatua zilizochukuliwa dhidi ya maofisa na askari wake waliohusika katika vitendo vya rushwa na unyanyasaji kwa wachimbaji wadogo wa madini huko Chunya mkoani Mbeya  mwishoni mwa mwezi Machi ,2019,” amesema Mwakatage

Amesema hawatakubaliana na ofisa au askari yeyote atakayechafua taswira ya jeshi hilo kwa vitendo vya rushwa na kunyanyasa wananchi.

Hivyo ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa makamanda wa zimamoto na ukoaji wa mikoa pindi wanapokutana na vitendo vyovyote wanavyovitilia shaka hususani kwenye shughuli za ukaguzi wa kinga na tahadhari dhidi ya moto unaofanywa na maofisa na askari  wa jeshi hilo.



Chanzo: mwananchi.co.tz