Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari wa JWTZ kortini akidaiwa kumpa mimba mwanafunzi

39789 Pic+mmba Askari wa JWTZ kortini akidaiwa kumpa mimba mwanafunzi

Mon, 4 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), ambaye ni mshauri wa msaidizi wa mgambo wilayani hapa, Ramadhani Hamisi (46) amefikishwa Mahakama ya wilaya kujibu mashtaka mawili ya kubaka na kumpa mimba mwanafunzi.

Askari huyo mkazi wa Kebanchabancha, alikamatwa Januari 25 na kuwekwa mahabusu baada ya kutajwa na mtoto huyo kuhusika na kitendo hicho kilichomsababishia kukatisha masomo yake.

Juzi, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ismael Ngaile, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Renatus Zakeo alidai kuwa Hamisi alitenda makosa hayo Juni, 2018.

Alidai alimbaka mwanafunzi huyo wa kidato cha nne mwenye umri wa miaka 17 aliyekuwa akisoma Sekondari ya Ikorongo mashtaka ambayo mshtakiwa huyo aliyakana yote .

Askari huyo yupo nje kwa dhamana baada ya kukidhi masharti yaliyotolewa na Hakimu Ngaile ya kuwa na wadhamini wawili, mmoja akiwa mtumishi na kila mmoja asaini dhamana ya maneno ya Sh9 milioni na kesi hiyo itatajwa tena Februari 27.

Anayedaiwa kuwa ofisa feki wa Necta

Mtu anayedaiwa kujifanya ofisa wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) aliyekamatwa Januari 25 akiendesha ukaguzi katika sekondari ya Serengeti Nuru, hajafikishwa mahakamani ikielezwa kuwa bado uchunguzi unaendelea ili kubaini mtandao wake.

Mtu huyo aliyejitambulisha kwa jina la Athumani Salum akijiita ni naibu katibu wa Necta, alipitia ofisi ya ofisa elimu mkoa na kuongozana na ofisa elimu taaluma sekondari, Elisanguo Mshiu hadi kwa ofisa elimu sekondari wilaya na kwenda Serengeti Nuru ambako alibanwa baada ya kubainika ni tapeli.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Juma Ndani alisema baada ya maofisa wa Necta ambao walifika Januari 30 kwa mahojiano kukamilisha kazi yao, atafikishwa mahakamani na wengine watakaokuwa wamehusika na tuhuma hizo.



Chanzo: mwananchi.co.tz