Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari polisi adaiwa kukatwa nyeti na mkewe

90559 RPC+Debora Askari polisi adaiwa kukatwa nyeti na mkewe

Thu, 2 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Shinyanga. Askari Polisi nchini Tanzania mwenye namba H. 8980 PC Kazimili (28) mkazi wa Shinyanga amenusurika kifo baada ya kujeruhiwa kwa kukatwa sehemu za siri na mke wake kwa kutumia kitu chenye ncha kali kwa kile kinachodaiwa ni wivu wa kimapenzi.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumatano Januari 1, 2020, Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Deborah Magiligimba amemtaja mwanamke anayedaiwa kutenda tukio hilo ni Flora Adam.

Kamanda Magiligimba amesema tukio hilo lilitokea saa 6:00 usiku wa kuamkia Desemba 28, 2019 nyumbani kwa wanandoa hao mtaa wa Uzunguni Manispaa ya Shinyanga nchini Tanzania.

Amesema mtuhumiwa anadaiwa kufanya tukio hilo wakati mume wake akiwa amelala.

“Mwanamke huyo alimvizia mume wake akiwa amelala muda wa saa 6:00 usiku na kuchukuwa kitu chenye ncha kali na kumkata sehemu  za siri," amesema

Kamanda huyo amesema," Mtuhumiwa anashikilliwa kwa mahojiano."

Amesema askari huyo alikimbizwa hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga alikotibiwa na kuruhusiwa baada ya hali yake kuimarika.

Chanzo: mwananchi.co.tz