Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari polisi, Afisa TRA wadakwa dawa za kulevya      

A7a5f186d1a94fe789f8ee09b8b1291d.jpeg Askari polisi, Afisa TRA wadakwa dawa za kulevya      

Mon, 19 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Askari Polisi na Raia katika msako dhidi ya madawa ya kulevya uliofanikiwa kunasa kilo 99.33 za dawa za kulevya katika kipindi cha mwezi Juni.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Gerald Kusaya aliwataja wahusika ambao ni Askari Polisi F. 6763 CPL Deodatus Leonid Massare (37) kabila mrangi, wengine ni Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Andrew Wailes Paul (45) kabila Muha, mkazi wa Kurasini na Ally Juma Ally (32) kabila Mzaramo, mkazi wa Kinyerezi mkoani Dar es Salama.

Akifafanua kukamtwa kwa watuhumiwa hao, Kamishna Jenerali Kusaya, alisema mapema mwezi Juni walikamata kilo 88.27 za dawa za kulevya zikiwa ndani ya gari aina ya Toyota Prado namba T 503 DHC ikiwa imetelekezwa Kimara Korogwe mkoani Dar es Salaam.

“Katika uchunguzi tuliofanya juu ya gari lililokamatwa, tulibaini kuna dawa nyingine ziliibiwa na baadhi wa yawatumishi wasio waaminifu ambao walishiriki uhalifu huo,” alisema Kusaya na kuongeza

“Hivyo Juni 18, katika eneo la Mburahati Madoto NHC tulifanikiwa kumkata mume na mke ambao ni Jamal Said Nangatukile (45) kabila Mmakonde, Mariyamu Rashid Bacha (28) kabila Mburushi wakiwa na dawa aina ya heroin yenye uzito wa gramu 494.52.

Kusaya amesema Juni 19, walimkataa askari Polisi F. 6763 CPL Deodatus Leonid Massare (37) kabila mrangi akiwa na kilo 1.04 ya dawa za kulevya aina ya heroin.

Aidha Kusaya alisema katika maeneo ya Mivinjeni Wilaya ya Temeke siku ya Juni 21 walimkatama Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Andrew Wailes Paul (45) kabila Muha, mkazi wa Kurasini na wenzake Said Rashid Mgoha (45) maarufu Kindimu kazi yake ni fundi gereji kabila Mkwere mkazi wa Mtoni Kijichi pamoja na George David Mwakang’ata (38) kabila Mnyakyusa, mfanyabiashara mkazi wa Mtoni Kijichi wakiwa na dawa za kulevya aina ya heroin kilo 1.02.

“Juni 23 tulimkamata Afrisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ally Juma Ally (32) kabila Mzaramo, mkazi wa Kinyerezi mkoani Dar es Salama pamoja na Abubakar Juma Abdall (28) kabila Mshiraz, mfanyabiashara wakiwa na dawa za kulevya aina ya Methamphetamine yenye uzito wa gramu 597.61.

Kusanya alisema baada ya kufanya upekuzi nyumbani kwa Ally maeneo ya Zimbili Kinyerezi alikutwa na pesa taslimu sh miloni 82.43 pamoja na Dola za Marekani 5,100.

“Watuhumiwa wote wameshafikishwa mahakamani wakikabiliwa na makosa ya kujihusisha na usafirishaji na biashara ya dawa za kulevya makosa ambayo ni uhujumu uchumi kwa sheria za nchi yetu,” alisema

Alisema pamoja na hatua hiyo ya kuwafikisha mahakamani bado wanaendelea na uchungiz ili kubaini wahalifu wengine walioshiriki katika tukio hilo.

“Natoa onyo kwa wale wanaotaka kujaribu makali ya serikali kwa kuendeleza au kujihusisha na biashara hii haramu, ninawaonya waachane na biashara hii na badala yake wajikite katika biashara na shughuli nyingine halali,” alisisitiza Kusanya.

Chanzo: www.habarileo.co.tz