Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari mbaroni akituhumiwa kwa mauaji

Mbaroniiiiiiiii Askari mbaroni akituhumiwa kwa mauaji

Fri, 8 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia askari wa wanyamapori kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Ngatipa Parmao (17) kwa madai ya kuswaga mifugo ndani ya Hifadhi ya Mkomazi.

Mtoto huyo ambaye ni wa jamii ya kimasai na mkazi wa kijiji cha Pangaroo, wilayani Mwanga anadaiwa kupigwa risasi Julai 6, 2022 na askari ambapo amefariki leo Katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) alikokuwa anapatiwa matibabu.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Abdalah Mwaipaya amekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba taarifa za kifo cha mtoto huyo wamezipokea leo asubuhi.

"Ni kweli tumepokea taarifa za kifo cha mtoto huyo lakini zaidi tunafuatilia kujua mazingira ya kifo chake   lakini taarifa zilizopo ni kwamba waliingiza mifugo kwenye hifadhi ambapo askari walimkamata ndipo alipoita wenzake wakaja na sime ikabidi askari afyatue risasi angani," amesema Mwaipaya

Amesema wanamshikilia askari huyo kwa mahojiano zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live