Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari magereza mwanamke aliyemtorosha jela mpenzi wake ajiua

Casey White.jpeg Casey White na Vicky White

Tue, 10 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Askari magereza wa kike ambaye alitoroka na mshukiwa wa mauaji kutoka jela ya Alabama, Marekani amefariki dunia baada ya kujipiga risasi baada ya wawili hao kukamatwa.

Vicky White, 58, alifariki hospitalini baada ya yeye na Casey White (hawana uhusiano wa kindugu), 38, kukamatwa huko Indiana kufuatia msako wa polisi.

Wawili hao walikuwa walitoroka katika gereza la Kaunti ya Lauderdale tarehe 29 Aprili.

Inaaminika kuwa walikuwa wapenzi. Kulingana na maafisa, walionekana mara ya mwisho alipokuwa akimsafirisha kwa kisingizo cha uongo cha matatizo ya afya ya akili.

Ilikuwa siku ya mwisho ya Bi White kazini kabla ya kustaafu. Alikuwa ameuza nyumba yake hivi majuzi na akawaambia wenzake kwamba alipanga kutumia wakati mwingi ufukweni.

Ofisi ya wachunguzi wa Kaunti ya Vanderburgh ilithibitisha kwamba Vicky White alifariki katika hospitali ya eneo hilo baada ya kujipiga risasi wakati wa kukamatwa.

Taarifa zaidi kuhusu kifo chake zinatarajiwa kutolewa leo Jumanne kufuatia uchunguzi wa maiti yake.

Sherifu wa Kaunti ya Lauderdale Rick Singleton alisema hapo awali kwamba gari la wapenzi hao hao lilipinduka wakiwa kwenye harakati za kutoroka baada ya msako wa polisi huko Evansville, Indiana, ambapo Casey White alijisalimisha.

"Tumemkamata mtu hatari mtaani leo. Hataona mwanga wa jua tena," alisema. Casey White alikuwa anatumikia miaka 75 jela kwa makosa mengine mbalimbali ikiwemo ya wizi aliyoyafanya mwaka 2015.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live