Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari magereza atoroka na mrembo anayetuhumiwa kwa mauaji

Casey White.jpeg Askari magereza atoroka na mrembo anayetuhumiwa kwa mauaji

Wed, 4 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Askari mmoja wa Jeshi la Magereza nchini Marekani, Vickey White mwenye umri wa miaka 56 pamoja na mahabusu anayeshukiwa kwa makosa ya mauaji, Casey White (38) wanaodaiwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi wametoroka na kuelekea kusikojulikana.

Askari huyo ndiye anadaiwa kusuka mpango wa kumsaidia mrembo huyo kutoroka gerezani kisha naye kutoroka na kwenda naye.

Taarifa kutoka ofisi ya mkuu wa polisi katika Jimbo la Alabama nchini humo inasema kwamba taarifa hizo zilitajwa na wafungwa wenzake ambapo msako wa kumtafuta mfungwa huyo pamoja na askari huyo unaendelea.

Imeelezwa kuwa wawili hao walitoroka wakati alipokuwa akimpeleka katika kituo bandia cha ukaguzi wa akili. Maofisa hatahivyo hawajathibitisha iwapo uhusiano huo ulikuwa wa kimapenzi.

Siku ya Ijumaa, siku ambayo wawili hao walitoroka ilikuwa siku ya mwisho ya kazi. Alikuwa ameiuza nyumba yake na kuwaambia wenzake kwamba alikuwa anapanga kuishi maisha yake katika ufukwe wa bahari.

Maofisa wa polisi sasa wanaamini kwamba askari Jela huyo alihusika katika kupanga kumtorosha mfungwa huyo baada ya kukiuka itifaki ya jela hiyo na kumsindikiza Casey akiwa pekee.

Wachunguzi walipokea habari kutoka kwa wafungwa wengine katika kituo cha Lauderdale County wikendi iliopita kwamba kulikuwa na uhusiano maalum kati ya Mkurugenzi White na mfungwa Casey White, Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Rick Singleton alisema katika taarifa yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live