Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari magereza Segerea wakamisha kesi vigogo wa Acacia

64730 Pic+accasia

Fri, 28 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kesi inayowakabili aliyekuwa Makamu Rais wa Kampuni ya uchimbaji Madini ya Acacia, Deogratius Mwanyika na wenzake imeshindwa kuletwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam nchini Tanzania kutokana na upungufu wa maofisa wa gereza la Segerea.

Wakili wa Serikali, Elia Athanas amedai leo Ijumaa Juni 28,2019 mahakamani hapo kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini washtakiwa hawajafika kutokana na baadhi ya askari wa gereza la  Segerea kwenda kwenye mafunzo na kusababisha uhaba wa askari

"Upelelezi haujakamilika na nimeambiwa baadhi ya maofisa wa gereza la Segerea wameenda kwenye mafunzo hivyo kutokana na upungufu wa askari wameshindwa kuwaleta washtakiwa hao," amedai Athanas.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kelvin Mhina amesema kutokana na upungufu wa askari wa magereza kutowaleta washtakiwa hao ameahirisha shauri hilo hadi Julai 8, 2019 itakapotajwa tena.

Mbali na Mwanyika washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu Alex Lugendo, Mkurugenzi Mtendaji wa Pongea, North Mara na Bulyanhuku Assa Mwaipopo, kampuni ya Mgodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu.

Wanadaiwa, walitenda makosa hayo kati ya Aprili 11, 2008 na Juni 30,2007 katika sehemu tofauti za jijini la Dar es Salaam, Kahama Mkoani Shinyanga, Tarime Mara, Biharamulo Kagera maeneo ambayo yapo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia Soma

Maeneo mengine ambayo washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo ni katika mji wa Johannesburg, Afrika Kusini, Toronto Canada na nchini Uingereza.

Aidha mshtakiwa Mwanyika na Lugendo, wanadaiwa kutoa msaada katika kusimamia mkakati wa kihalifu kwa nia ya kupata faida.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutoa tamko la uongo kwa kamishna jenerali wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) huko Biharamulo kwa nia ya kukwepa kulipa kodi ya USD 9,309,600 ambayo ilikuwa ni kodi iliyopaswa kulipwa kwa TRA.

Washtakiwa Mwanyika na Lugendo wanadaiwa kati ya Desemba 2009 na Desemba 31 2018 katika maeneo tofauti ndani na nje ya nchi ya Tanzania kwa pamoja na wengine ambao hawapo mahakamani, walisaidia mgodi wa North Mara kuhamisha fedha kiasi cha USD 374,243,943,45 huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la makosa ya kughushi na kukwepa kodi.

Chanzo: mwananchi.co.tz