Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari anayetuhumiwa kumpiga mtuhumiwa atiwa mbaroni

IMG 20220823 WA0198 Askari anayetuhumiwa kumpiga mtuhumiwa atiwa mbaroni

Tue, 23 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi nchini Tanzania linamshikilia askari mmoja kwa kosa la kumpiga kijana aliyekuwa amefungwa pingu mkononi, kitendo kinachotafsiriwa kama kinyume cha sheria

Hatua hiyo inakuja baada ya video ya kijana huyo kusambaa katika mitandao ya kijamii na kuleta maoni mbalimbalimiongoni watumiaji wa mitandao.

Katika taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime imesema kuwa kijana huyo anayeonekana katika video hiyo akipigwa na pingu mkononi, alituhumiwa kwa kuiba simu na alikiri kosa hilo na kwenda kuonyesha mtu aliyemuuzia ambaye alikutwa na simu hiyo.

"Kitendo hicho si tu kwamba ni kinyume cha sheria bali pia ni kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi, tukio limesha chukuliwa hatua kuanzia jana" alisema

Kwa mujibu wa Jeshi la polisiwanasema tukio hilo limeshachukuliwa hatua na Polisi Kinondoni na 'askari aliyehusika yupo mahabusu na hatua stahiki zinaendelea kuchukuliwa'

Jeshi hilo limesema kuwa litaendelea kuchukua hatua stahiki dhidi ya askari Polisi anayekiuka sheria ya maadili ya Jeshi la Polisi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live