Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari anayedaiwa kukutwa na heroini ngoma nzito

Madawa Piv Askari anayedaiwa kukutwa na heroini ngoma nzito

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: mwanachidigital

Askari wa vikosi vya ulinzi na usalama vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Juma Abdalla Khamis (34) anayedaiwa kukamatwa akisafirisha dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Pemba amegoma kutaja mtandao wake.

Hata hivyo, askari huyo bado yupo chini ya ulinzi wakati taratibu za kumpeleka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) zikiendelea.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu jana, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Zanzibar, Kanali Burhan Zubei Nassor alisema “bado hajafunguka (kuwataja), tunaendelea na upelelezi, ameendelea kuwa chini ya ulinzi, tupo kwenye hatua za kumpeleka kwa DPP,” alisema Burhan. Related

Askari akamatwa na dawa za kulevya Zanzibar Kitaifa 1 hour ago Mzee wa miaka 74 akamatwa Uwanja wa Ndege akisafirisha dawa za kulevya Kitaifa 1 hour ago

Askari huyo alikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Dawa za Kulevya Aprili 11, 2023 akiwa na vifuko 31 vyenye kete 3,198 zinazodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya aina ya heroini.

Kwa mujibu wa kamisha huyo, bila kutaja askari huyo ni mtumishi wa kikosi gani kutokana na upelelezi, alikamatwa na maofisa wa mamlaka hiyo saa 10:30 jioni katika uwanja wa ndege Pemba.

Bado haijajulikna alikuwa anasafirisha mzigo huo kwenda wapi na wateja wake ni kina nani.

Mtuhumiwa ni mkazi wa Kibanda Maiti Unguja.

Hali ilivyo

Septemba mwaka jana Athumani Akida Juma (32) mkazi wa Nungwi alikamatwa na pakiti 20 zenye kete 2,401 zinazodaiwa ni dawa za kulevya aina ya heroini.

Pia, Februari mwaka huohuo, Jeshi la polisi liliwakatama wanawake wawili kilo 5.62 za heroini katika uwanaj wa ndege wa kimataifa wa Abeid Aman Karume.

Kijana huyo alikamatwa katika operesheni na doria za ukamataji wahalifu wanojihusisha na dawa ya kulevya nchini.

Katika operesheni hiyo walikamata mzigo kisiwani Pemba uliotelekezwa ukiwa na kete 4,000 za bangi huku upelelezi ukiendelea kwa kutafuta mwenye mzigo huo.

Twakimu za mamlaka hiyo zilizotolewa Septemba mwaka jana, kesi 215 zinazohusu dawa hizo zilikuwa katika hatua mbalimbali katika vyombo vya sheria.

Mamlaka hiyo ilianza kufanya kazi Machi mwaka jana ikiwa na mamlaka ya kukamata, kupeleleza na kushtaki baada ya kufanyiwa marekebisho ya sheria ambayo awali ilionekana kutokuwa na meno ya kufanya hivyo.

Mmoja wa vijana waliowahi kuwa watumiaji wa dawa hizo baadaye kuacha, Issa Muhdin issa alisema mtandao wa dawa za kulevya nchini ni mkubwa na iwapo mamlaka itataka kufanikiwa haina budi kuwashirikisha vijana hao.

Chanzo: mwanachidigital