Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari aliyetuhumiwa kumjeruhi mtoto aachiwa huru

Hukumu Pc Data Askari aliyetuhumiwa kumjeruhi mtoto aachiwa huru

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu imemwachia huru askari, Abati Benedicto wa Kituo cha Polisi Bariadi alyekuwa akikabiliwa na kesi ya kumpiga hadi kumjeruhi mtoto wake mwenye umri wa miaka saba.

Katika hukumu iliyosomwa Machi 20, 2024 na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Caroline Kiliwa amesema mahakama imemwachia huru mtuhumiwa kutokana na vielelezo vya ushahidi vilivyoletwa mahakamani hapo na upande wa mashtaka kushindwa kumtia hatiani.

Hakimu Kiliwa amesema kuwa mmoja wa mashahidi wa upande wa mashtaka alikuwa daktari, ambapo maelezo yake yalieleza kuwa wakati anamtibu mtoto alimkuta na tatizo la upungufu wa damu mwilini, mchafuko wa damu pamoja na kuvimba miguu.

“ Ukimsikiliza daktari hakuna sehemu yeyote ambayo alisema chanzo cha magonjwa hayo ya mtoto ni kupigwa na Baba yake tena kwa fimbo, lakini mtoto mwenyewe alisema alipigwa mara moja tu, Je tunajiuliza kupigwa mara moja na hayo magonjwa na majeraha yote aliyokuwa nayo mtoto?“ amesema Hakimu Kiliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live