Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari alazwa hospitali akidai kuvutishwa bangi na vibaka

Msokoto Wa Bangi Bangi Bangi Askari alazwa hospitali akidai kuvutishwa bangi na vibaka

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni, kauli hii inaendana na kisa kilichomtokea Ofisa wa Polisi anayedaiwa kulazimishwa kuvuta bangi na genge la vibaka nchini Kenya.

Tovuti ya Taifa na Tuko zimeripoti kuwa inadaiwa askari huyo alikuwa katika doria kabla ya kukutwa na mkasa huo uliotokea eneo la Kayole, Kaunti ya Murang’a nchini Kenya, jana Jumamosi, Februari 3, 2024.

Inadaiwa askari huyo alikuwa na wenzake wakati wa msako eneo la Kayole uliokuwa na nia ya kusambaratisha mtandao wa wauzaji na watumiaji wa bangi.

Tovuti ya Tuko inaeleza ulizuka ugomvi kati ya askari hao pamoja na genge hilo, hali iliyowafanya wenzake wawili kukimbia na kumuacha akikumbwa na masaibu hayo ya kupewa msokoto wa bangi.

Kwa sasa askari huyo amelazwa Hospitali Kuu ya Murang’a. Mkuu wa Polisi wa Murang’a Mashariki, Mary Wakuu, amethibitisha kisa hicho na kueleza uchunguzi unaendelea.

Mkuu huyo wa Polisi amesema msako utafanywa, ili kuwakamata watu hao na kuongeza kuwa eneo hilo linachunguzwa kwa matumizi ya bangi.

"Ni eneo ambalo tunapaswa kulisafisha. Pia nawaonya polisi watekeleze wajibu wao kwa busara na uadilifu. Mambo haya yote yatachunguzwa na ripoti ya kina itaandaliwa," amesema Kamanda Mary.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live