Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari Polisi, wengine watatu mbaroni wizi IPTL

CB28E313 D02F 4582 A25A BB6306DF2B09.jpeg Askari Polisi, wengine watatu mbaroni wizi IPTL

Sat, 11 Mar 2023 Chanzo: Mwananchi

Baadhi ya mitambo ya kampuni binafsi ya kufua umeme (IPTL) inadaiwa kuibiwa na watu wanne akiwemo askari Polisi aliyekuwepo lindo siku ya tukio.

Mitambo hiyo iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam, ilisitishwa kutoa huduma ya kuzalisha umeme kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) mwaka 2013 baada ya kutoelewana kwa wahusika wa mkataba wa makubaliano.

Kulingana na taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii, watuhumiwa wa tukio hilo wanashikiliwa na Polisi katika Kituo cha Oysterbay jijini hapa.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amethibitisha tukio hilo.

“Tumezipata taarifa hizo na tunazichunguza katika uchunguzi kuna watu wanahojiwa,” ameeleza kwa ufupi bila kufafanua kwa kina.

Chanzo: Mwananchi