Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari Polisi, JWTZ kizimbani wakidaiwa kuiba mafuta ya ATCL

75136 Askari+pic

Tue, 10 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Askari watano wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania na mwanajeshi mmoja wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo wizi wa mafuta ya ndege na utakatishaji wa  fedha zaidi ya Sh4.6 milioni.

Washtakiwa katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 93/2019 ni Koplo Shwahiba (38), MT. 74164 SGT Ally Chibwana (47) wa JWTZ, PC Elidaima Paranjo (38), PC Simon (28), PC Dickson  na PC Hamza.

Akisoma hati ya mashtaka leo Jumanne Septemba 10,2019 mbele ya Hakimu Mkazi, Vicky Mwaikambo,  Wakili wa Serikali Faraji Nguka akisaidiana na Saada Mohammed amedai washtakiwa wote hao wakiwa ni watumishi wa umma walikiuka maadili ya kazi zao na kupanga genge la uhalifu na kuiba lita 2,180 za mafuta ya ndege (Jet A-1/Ik yenye thamani ya sh. 4,647,760.

Katika shtaka la pili, inadaiwa, Julai 30, 2019 katika uwanja wa ndege wa  Julius Nyerere Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, watuhumiwa hao,  waliiba lita 2,180 za mafuta ya ndege aina ya (Jet A-1/Ik yenye thamani ya Sh4,647,760 mali ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)

Shtaka la tatu, imedaiwa siku na eneo hilohilo washtakiwa wote kwa pamoja walifanya wizi wa mafuta hayo na kutakatisha fedha kiasi cha Sh4.6 milioni ambapo wakijua fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la wizi kinyume na sheria.

Hata hivyo, baada ya kusomewa mashtaka hayo, hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

Pia Soma

Advertisement
Washtakiwa hao wanatetewa na Wakili Hasaan Kiangio.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 24 kesi itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa wote wamerudishwa rumande.

Chanzo: mwananchi.co.tz