Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari JWTZ mbaroni akidaiwa kumuua mzazi mwenzake na bosi

33906 Pic+askari Tanzania Web Photo

Sat, 29 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Songea. Polisi mkoani Ruvuma inamshikilia askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kikosi cha Chandarua, Batisin Samda kwa tuhuma za kumuua kwa risasi mzazi mwenzie Veronica Kayombo na mtu mwingine anayedaiwa kuwa bosi wake, Juma Mkele akiwa kazini.

Wakati askari huyo akidaiwa kutekeleza tukio hilo, askari Magereza wa Gereza la Kitai wilayani Mbinga mkoani humo, Adam Maganga amefariki dunia baada ya kujipiga risasi kichwani akiwa lindoni.

Akizungumza na Mwananchi jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Gemin Mushy alisema tukio alilotekeleza Samda lilitokea juzi saa kumi jioni katika kambi ya JWTZ Chandarua iliyopo katika Manispaa ya Songea.

Alisema uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea na mtuhumiwa yupo mahabusu huku miili ya marehemu wote wawili ikiwa imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya uchunguzi wa daktari.

Kamanda huyo alisema katika tukio la askari Magereza, Maganga, chanzo cha tukio bado kinachunguzwa.

Kufuatia matukio hayo, Kamanda Mushy amewaonya wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi akisisitiza kuwa wakibainika watafikishwa mahakamani.



Chanzo: mwananchi.co.tz