Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari JWTZ ashikiliwa kwa tuhuma ya kubaka

38379 ASKARI+PIC Askari JWTZ ashikiliwa kwa tuhuma ya kubaka

Fri, 25 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Watu watatu akiwamo askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kubaka watoto, huku mmoja akidaiwa kufanya hivyo kwa mtoto wake wa kumzaa na mwingine watoto wake wa kufikia.

Akizungumzia matukio hayo jana, kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Wilbrod Mutafungwa alidai askari mmoja wa JWTZ kambi ya Suku Mikumi anashikiliwa na polisi kwa tuhuma ya kufanya mapenzi na binti wa miaka 17 mwanafunzi wa kidato cha nne.

Alisema askari huyo alikamatwa Januari 23 mwaka huu majira ya alasiri maeneo ya Kikwalaza Mikumi wilaya ya Kilosa.

“Askari huyo alikamatwa na wananchi na kumfikisha katika kituo cha polisi Mikumi baada ya kumwita mwanafunzi huyo na rafiki yake nyumbani kwake kwa nia ya kufanya naye mapenzi kinyume cha sheria,” alisema.

Katika tukio jingine, kamanda Mutafungwa alisema mkazi wa Mikumi (68) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwabaka watoto wawili wa familia moja,mmoja mwenye umri wa miaka nane na mwingine tisa ambao ni watoto wake wa kufikia.

Kamanda Mutafungwa alisema mtuhumiwa huyo aliwabaka watoto hao baada ya kuwatoa ndani walikolala na kuwapeleka nyuma ya nyumba huku akiwatishia kuwapiga.

Wakati huohuo, polisi wanamshikilia mkazi wa Kidudwe Turiani kwa tuhuma ya kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka sita baada ya kumwita chumbani.

Kamanda Mutafungwa alisema tukio hilo lilitokea Januari 21 mwaka huu saa 4:00 asubuhi katika kijiji cha Kidudwe Turiani, ambapo mama mzazi wa mtoto huyo aligundua kuwa mtoto wake amebakwa na hivyo kutoa taarifa polisi. Alisema watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi na taratibu za kisheria kukamilika.



Chanzo: mwananchi.co.tz