Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari JWTZ akutwa ameuawa kwenye mashamba ya mkonge Morogoro

63579 Mashambapic

Thu, 20 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kikosi cha Pangawe mkoani Morogoro, Leonald Liumba (52) ameuawa na mwili wake kukutwa umetupwa kwenye mashamba ya Mkonge ya Tungi.

Kutokana na mauaji hayo, Polisi mkoani hapa wanawashikilia watu watatu  kwa tuhuma za mauaji hayo.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Wilbroad Mutafungwa leo Jumatano Juni 19, 2019 aliwaambi waandishi wa habari kuwa tukio lilitokea Mei 30, 2019 saa nne asubuhi eneo la  Tungi katika mashamba ya mkonge Manispaa ya Morogoro ulikokutwa mwili huo ukiwa umetupwa.

Kamanda huyo amesema askari alitoweka nyumbani kwake tangu Mei, 25 mwaka huu.

Amesema mwili wake umekutwa umefungwa kamba mikononi na miguuni huku ukiwa na majeraha eneo la kisogoni na umeanza kuharibika.

Amewataja watuhumiwa ni Charles Luhunga maarufu Ubaya (36) na mwendesha bodaboda mkazi wa Msamvu Morogoro, Juma Said (25) maarufu Sokomoko mfanyabiashara katika Soko la Kikundi na Yusuph Makusi (24), mwendesha bodaboda eneo la Msamvu Morogoro na Dar es Salaam.

Pia Soma

 

Chanzo: mwananchi.co.tz