Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari JWTZ aendelea kusota rumande

Tue, 19 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Ramadhan Mlaku (28) anayekabiliwa na kesi ya mauaji anaendelea kusota rumande kutokana na upelelezi wa shauri hilo kutokamilika.

Wakili wa Serikali, Daisy Makakala amedai leo Jumatatu Machi 18, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

“Shauri hili limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika, naiomba mahakama hii ipange tarehe nyingine,” amedai Makakala.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili Mosi, 2019 itakapotajwa tena na mshtakiwa amerudishwa rumande kutokana na shtaka hilo kutokuwa na dhamana.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Mlaku anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 30, 2017, eneo la Upanga, makao makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam.

Mlaku ambaye ni mwanajeshi wa kambi ya Jeshi hilo iliyopo Makongo, anadaiwa kumuua mwanajeshi mwenzake Sajenti Saimon Munyama.



Chanzo: mwananchi.co.tz